Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAENDELEA KUTOA FURSA ZA “INTERNSHIP” KWA WANAFUNZI WA VYUO MBALIMBALI APA NCHINI

  • September 7, 2023

DAR ES SALAAM.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yatembelewa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali kutoka Chuo Cha Usafirishaji (NIT), Chuo Cha Ardhi (ARU), Chuo Cha Tumaini (TUDARCO) na Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) tarehe 06 Septemba, 2023 katika kumbi zilizopo ndani ya Taasisi.


Wanafunzi hao wamepata elimu kuhusu Majukumu ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ambapo Afisa Biashara TanTrade Bi. Eliza John Haule aliwaelimisha kuhusu  umuhimu wa Rajamu (Branding) kwa bidhaa na huduma na mbinu mbalimbali za kufanikisha ufaulu wa rajamu katika biashara.


Kadhalika, Afisa Biashara TanTrade Bi. Leah John Msaga ameweza kujibu maswali mbalimbali na kutoa ufafanuzi zaidi ya mambo ambayo wanafunzi hao walikuwa na matarajio ya kujua, ambapo Afisa Operesheni wa Mutual Generation International Institute Bi. Diana Godfrey Nyangoma aliweza kupata ufafanuzi kuhusu mchanganuo mzima wa uzalishaji na uagizaji bidhaa nchini.


Wanafunzi hao wametoa shukrani za dhati kwa kupokelewa vizuri na wameweza kujifunza vitu mbalimbali kuhusu Taasisi hasa katika mchango wake katika kuwasaidia wafanyabiashara kufikia malengo ya ukuaji kiuchumi ndani na nje ya nchi